Technician

Welcome to this internet site

Archive for the 'Swahili/Kiswahili' Category

Mfalme Mumbere ashtakiwa kwa mauaji wilayani Kasese nchini Uganda

Posted by technician on 30th novembre 2016

media

Silaha zilizopatikana katika Ufalme wa Rwenzururu

Mfalme wa eneo la Rwenzururu nchini Uganda Charles Mumbere amefunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya watu 87 kupoteza maisha mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya makabiliano kati ya maafisa wa usalama na walinzi wake.

Mumbere alikamatwa akiwa siku ya Jumamosi na kusafirishwa mjini Jinja ambako amekuwa akizuiliwa, lakini amekanusha kuhusika na machafuko hayo.

Serikali ya Uganda inamtuhumu kuwa anaunda kundi la waasi kwa lengo la kutaka kuunda nchi yake itakayoitwa Yiira

Mfalme huyo anatarajiwa kurudi Mahakamani katikati ya mwezi Desemba.

Wachambuzi wa siasa nchini Uganda wanahisi kuwa mgogoro wa Ufalme huu unatokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kutengwa kimaendeleo kwa muda mrefu na suala la uongozi.

Suala la ardhi limekuwa tata sana katika eneo hilo, asilimia 60 ya ardhi katika Wilaya ya Kasese inamilikiwa na serikali na hivyo haiwanufaishi watu wa eneo hilo.

Licha ya Wilaya hiyo kuwa na utajiri wa rasilimali kama Ziwa Katwe, George na Edward. Madini mbalimbali na viwanda kama kile cha Hima, watu wengi katika Wilaya ya Kasese wanaendelea kuishi kwa umasikini na hawana ajira hasa vijana.

Jambo lingine la kutilia maanani ni kuwa eneo la Kasese na Rwenzori lina idadi kubwa ya wapiganaji walioshiriki katika vita dhidi ya Ufalme wa Tooro miaka ya 1960 lakini pia kumsaidia Museveni wakati wa vita vya msituni na sasa hivi wanahisi kuwa hawajalipwa chochote wala kukumbukwa kwa namna yoyote ile.

  Posted in Swahili/Kiswahili | No Comments »

  Rubavu: Muganga wa chenyeji ametiwa mbaroni

  Posted by technician on 23rd novembre 2016

  Muganga wa chenyeji ametiwa mbaroni

  Polisi ya Rwanda katika wilaya ya Rubavu imekamata Dusengimana Felicien mwenye umri wa miaka 39 akihukumiwa kuwadanganya watu kwamba yeye ni muganga wa chenyeji huku anatibu magonjwa tofauti.

  Tarehehe 21 Novemba 2016 katika kata ya Nyakiriba, nyumbani kwake mganga palitokea kelele kubwa kwa sabau wagonjwa wawili walipigana , na palikuwepo wagonjwa 17, raia wa sehemu hiyo walipo sikia kelele waliambia polisi na ndipo msaada ulipatikana kwa gafla.

  CIP Theobald Kanamugire msemaji wa polisi katika jimbo la magharibi alisema, “Bwana huyu anayejiita mganga wa chenyeji amewadanganya watu wengi na kusema kwamba yeye ana mamlaka ya kutibu magonjwa mengi”.

  Polisi huendelea na kusema kwamba Dusengimana mwenye umri wa miaka 39 ana watoto wawili, na wagongwa wote 17 walikua wakiishi kwake na walikua wakilipa hata chakula ambacho alikua akiwatayarishia, na walipomshika wale wagonjwa wote walipelekwa hospitalini ili wapate matibabu kamili.

  Baada ya upelelezi mshutumiwa akishikwa na makosa ataazibiwa kufungwa kati wa mwaka mmoja na miaka tatu na kutoa garama karibu miliyoni moja ya pesa za Rwanda.

  Posted in Swahili/Kiswahili | No Comments »

   


  Créer un Blog | Nouveaux blogs | Top Tags | 493 articles | blog Gratuit | Abus?